Ayu. 32:10-22 Swahili Union Version (SUV)

10. Basi nilisema, Nisikilizeni mimi;Mimi nami nitawaonyesha nionavyo.

11. Tazama, niliyangojea maneno yenu,Nilizisikiliza nisikie hoja zenu,Hapo mlipokitafuta mtakalonena.

12. Naam, niliwasikiza ninyi,Na tazama, hapana mmoja aliyemshinda Ayubu,Wala kumjibu maneno yake, kati yenu.

13. Jitunzeni msiseme, Sisi tumepata hekima;Mungu yumkini akamshinda, si mtu;

14. Kwa kuwa yeye hajayaelekeza maneno yake kwangu;Wala sitamjibu mimi kwa maneno yenu.

15. Wameshangaa, hawajibu tena;Hawana neno la kusema.

16. Na mimi, je! Ningoje, kwa sababu hawaneni,Kwa sababu wasimama kimya, wala wasijibu tena;

17. Mimi nami nitajibu sehemu yangu,Mimi nami nitaonyesha nionavyo.

18. Kwa kuwa nimejaa maneno;Roho iliyo ndani yangu hunihimiza.

19. Tazama, tumbo langu ni kama divai iliyozibwa;Kama viriba vipya li karibu na kupasuka.

20. Nitanena, ili nipate kutulia;Nitafunua midomo yangu na kujibu.

21. Tafadhali, nisiupendelee uso wa mtu;Wala sitajipendekeza kwa mtu ye yote.

22. Kwani mimi sijui kujipendekeza;Au Muumba wangu angeniondoa kwa upesi.

Ayu. 32