Ayu. 31:9-14 Swahili Union Version (SUV)

9. Kama moyo wangu ulishawishwa kwa mwanamke,Nami nimeotea mlangoni pa jirani yangu;

10. Ndipo hapo mke wangu na asage kwa mwingine,Na wengine na wainame juu yake.

11. Kwani hilo lingekuwa kosa kuu;Naam, lingekuwa ni uovu wa kuadhibiwa na waamuzi;

12. Kwa kuwa ni moto uteketezao hata Uharibifu,Nao ungeyang’oa maongeo yangu yote.

13. Kama nimeidharau daawa ya mtumishi wangu, au ya kijakazi changu,Waliposhindana nami;

14. Basi Mungu atakapoinuka nitafanya nini?Naye atakapozuru, nitamjibuje?

Ayu. 31