7. Kwamba hatua yangu imekengeuka na kuiacha njia,Na moyo wangu kuyaandama macho yangu,Tena kwamba kipaku cho chote kimeshikamana na mikono yangu;
8. Basi na nipande, mwingine ale;Naam, mazao ya shamba langu na yang’olewe.
9. Kama moyo wangu ulishawishwa kwa mwanamke,Nami nimeotea mlangoni pa jirani yangu;
10. Ndipo hapo mke wangu na asage kwa mwingine,Na wengine na wainame juu yake.
11. Kwani hilo lingekuwa kosa kuu;Naam, lingekuwa ni uovu wa kuadhibiwa na waamuzi;
12. Kwa kuwa ni moto uteketezao hata Uharibifu,Nao ungeyang’oa maongeo yangu yote.
13. Kama nimeidharau daawa ya mtumishi wangu, au ya kijakazi changu,Waliposhindana nami;
14. Basi Mungu atakapoinuka nitafanya nini?Naye atakapozuru, nitamjibuje?
15. Je! Huyo aliyenifanya mimi ndani ya tumbo, siye aliyemfanya na yeye?Si yeye mmoja aliyetufinyanga tumboni?