Ayu. 31:35-40 Swahili Union Version (SUV)

35. Laiti ningekuwa na mtu wa kunisikia!(Tazama, sahihi yangu ni hii, Mwenyezi na anijibu);Laiti ningekuwa na hayo mashitaka yaliyoandikwa na adui yangu!

36. Hakika ningeyachukua mabegani;Ningejifungia mfano wa kilemba.

37. Ningemwambia hesabu ya hatua zanguNingemkaribia kama vile mkuu.

38. Kama nchi yangu yalia juu yangu,Na matuta yake hulia pamoja;

39. Kama nimeyala matunda yake pasipo kulipa,Au kama nimewafanya wenyewe kupotewa na uhai;

40. Miiba na imee badala ya ngano,Na magugu badala ya shayiri.Maneno ya Ayubu yamekoma hapa.

Ayu. 31