Ayu. 31:27-36 Swahili Union Version (SUV)

27. Na moyo wangu umeshawishwa kwa siri,Na midomo yangu imeubusu mkono wangu;

28. Hilo nalo lingekuwa uovu wa kuadhibiwa na waamuzi;Kwani ningemwambia uongo Mungu aliye juu.

29. Kama nilifurahi kwa kuangamia kwake huyo aliyenichukia,Au kujitukuza alipopatikana na maovu;

30. (Naam, sikukiacha kinywa changu kufanya dhambiKwa kuutaka uhai wake kwa kuapiza);

31. Kama watu wa hemani mwangu hawakunena,Ni nani awezaye kumpata mtu asiyeshibishwa na yeye kwa nyama?

32. Mgeni hakulala njiani;Lakini nilimfungulia msafiri milango yangu;

33. Ikiwa kama mwanadamu nimeyafunika makosa yangu,Kwa kuuficha uovu wangu kifuani mwangu;

34. Kwa sababu niliwaogopa mkutano mkubwa,Na dharau la jamaa lilinitia hofu,Hata nilinyamaa kimya, nisitoke mlangoni-

35. Laiti ningekuwa na mtu wa kunisikia!(Tazama, sahihi yangu ni hii, Mwenyezi na anijibu);Laiti ningekuwa na hayo mashitaka yaliyoandikwa na adui yangu!

36. Hakika ningeyachukua mabegani;Ningejifungia mfano wa kilemba.

Ayu. 31