Ayu. 30:5-12 Swahili Union Version (SUV)

5. Hufukuzwa watoke kati ya watu;Huwapigia kelele kama kumpigia mwivi.

6. Lazima hukaa katika mianya ya mabonde,Katika mashimo ya nchi na ya majabali.

7. Hulia kama punda vichakani;Hukusanyika chini ya upupu.

8. Wao ni wana wa wapumbavu, naam, watoto wa wahuni;Walifukuzwa kwa mijeledi watoke katika nchi.

9. Na sasa mimi nimekuwa wimbo wao,Naam, nimekuwa simo kwao.

10. Wao hunichukia, na kujitenga nami,Hawaachi kunitemea mate usoni.

11. Kwani ameilegeza kamba yake, na kunitesa,Wala hawajizuii tena mbele yangu.

12. Kwa mkono wangu wa kuume huinuka kundi;Huisukuma miguu yangu kando,Na kunipandishia njia zao za uharibifu.

Ayu. 30