Ayu. 30:4-7 Swahili Union Version (SUV)

4. Hung’oa mboga ya chumvi kwenye kichaka;Na mizizi ya mretemu ni chakula chao.

5. Hufukuzwa watoke kati ya watu;Huwapigia kelele kama kumpigia mwivi.

6. Lazima hukaa katika mianya ya mabonde,Katika mashimo ya nchi na ya majabali.

7. Hulia kama punda vichakani;Hukusanyika chini ya upupu.

Ayu. 30