Ayu. 30:16-23 Swahili Union Version (SUV)

16. Sasa nafsi yangu inamwagika ndani yangu;Siku za mateso zimenishika.

17. Wakati wa usiku mifupa yangu huchomeka ndani yangu,Na maumivu yanayonitafuna hayapumziki.

18. Kwa ugonjwa wangu kuwa na nguvu nyingiMavazi yangu yameharibika;Hunikaza kama shingo ya kanzu yangu.

19. Yeye amenibwaga topeni,Nami nimekuwa kama mavumbi na majivu.

20. Nakulilia wewe, wala huniitikii;Nasimama, nawe wanitazama tu.

21. Wewe umegeuka kuwa mkali kwangu;Nawe waniudhi kwa uweza wa mkono wako.

22. Waniinua juu hata upeponi, na kunipandisha juu yake;Nawe waniyeyusha katika dhoruba.

23. Kwani najua kuwa utanileta hata kifoni,Niifikilie nyumba waliyoandikiwa wenye uhai wote.

Ayu. 30