Ayu. 3:13-20 Swahili Union Version (SUV)

13. Maana hapo ningelala na kutulia;Ningelala usingizi; na kupata kupumzika;

14. Pamoja na wafalme na washauri wa dunia,Hao waliojijengea maganjoni;

15. Au pamoja na wakuu wenye dhahabu,Waliozijaza fedha nyumba zao;

16. Au, kama kuzikwa mimba iliyoharibika, nisingekuwako;Kama wachanga wasiouona mwanga kabisa.

17. Huko waovu huacha kusumbua;Huko nako hao waliochoka wapumzika

18. Huko wafungwa waona raha pamoja;Hawaisikii sauti yake msimamizi.

19. Wakuu na wadogo wako huko;Mtumishi yu huru kwa bwana wake.

20. Mbona yeye aliye mashakani kupewa mwanga,Na hao wenye uchungu rohoni kupewa uhai;

Ayu. 3