Ayu. 3:1-4 Swahili Union Version (SUV)

1. Baada ya hayo Ayubu akafunua kinywa chake, na kuilaani siku yake.

2. Ayubu akajibu, na kusema;

3. Na ipotelee mbali ile siku niliyozaliwa mimi,Na ule usiku uliosema,Mtoto mume ametungishwa mimba.

4. Siku hiyo na iwe giza;Mungu asiiangalie toka juu,Wala mwanga usiiangazie.

Ayu. 3