Ayu. 24:5-10 Swahili Union Version (SUV)

5. Tazama, kama punda-mwitu jangwaniWao hutoka kwenda kazini mwao, wakitafuta chakula kwa bidii;Jangwa huwapa chakula cha watoto wao.

6. Hukata nafaka zao mashambani;Na kuokota zabibu za waovu.

7. Hujilaza usiku kucha uchi pasipo nguo,Wala hawana cha kujifunika baridi.

8. Hutota kwa manyunyo ya milimani,Na kuambatana na jabali kwa kukosa sitara,

9. Wako wamwondoao matitini kwa nguvu huyo asiye na baba,Na kutwaa rehani kwa maskini;

10. Hata wazunguke uchi pasipo mavazi,Nao wakiwa na njaa huchukua miganda;

Ayu. 24