Ayu. 24:16-24 Swahili Union Version (SUV)

16. Wao hutoboa nyumba gizani;Hujifungia ndani wakati wa mchana;Hawaujui mwanga.

17. Kwani asubuhi kwao wote ni kama giza tupu;Kwani wao wavijua vitisho vya hiyo giza tupu.

18. Mwasema, Yeye ni mwepesi juu ya uso wa gharika;Sehemu yao inalaaniwa duniani;Hageuki kwenda njia ya mizabibuni.

19. Chaka na hari hukausha maji ya theluji;Kuzimu nako hao ambao wamefanya dhambi.

20. Tumbo lililomzaa litamsahau; buu litamla na kuona tamu;Hatakumbukwa tena;Na udhalimu utavunjwa kama mti.

21. Naam, yeye huwala walio tasa wasiozaa;Wala hamtendei mema mwanamke mjane.

22. Lakini Mungu huwadumisha wenye uwezo kwa nguvu zake;Huinuka, wasiokuwa na tumaini la kuishi.

23. Huwapa kuwa na salama, nao wapumzika kwayo;Na macho yake ya juu ya njia zao.

24. Wao wametukuzwa; lakini kitambo kidogo hutoweka;Naam, hushushwa, na kuondolewa njiani kama wengine wote,Nao hukatwa kama vile masuke ya ngano.

Ayu. 24