14. Mwuaji huamka asubuhi kukipambauka, huwaua maskini na wahitaji;Tena wakati wa usiku yu kama mwivi.
15. Tena jicho lake mzinifu hungojea wakati wa giza-giza,Akisema, Hapana jicho litakaloniona;Naye huuficha uso wake.
16. Wao hutoboa nyumba gizani;Hujifungia ndani wakati wa mchana;Hawaujui mwanga.
17. Kwani asubuhi kwao wote ni kama giza tupu;Kwani wao wavijua vitisho vya hiyo giza tupu.
18. Mwasema, Yeye ni mwepesi juu ya uso wa gharika;Sehemu yao inalaaniwa duniani;Hageuki kwenda njia ya mizabibuni.
19. Chaka na hari hukausha maji ya theluji;Kuzimu nako hao ambao wamefanya dhambi.
20. Tumbo lililomzaa litamsahau; buu litamla na kuona tamu;Hatakumbukwa tena;Na udhalimu utavunjwa kama mti.
21. Naam, yeye huwala walio tasa wasiozaa;Wala hamtendei mema mwanamke mjane.
22. Lakini Mungu huwadumisha wenye uwezo kwa nguvu zake;Huinuka, wasiokuwa na tumaini la kuishi.