10. Hata wazunguke uchi pasipo mavazi,Nao wakiwa na njaa huchukua miganda;
11. Hushindika mafuta ndani ya makuta ya watu hao;Wakanyaga mashinikizo, nao wana kiu.
12. Watu huugua toka mji ulio na watu wengi,Na roho yake aliyejeruhiwa hupiga ukelele;Wala Mungu hauangalii upumbavu.
13. Hawa ni katika hao waliouasi mwanga;Hawazijui njia zake,Wala hawakai katika mapito yake.
14. Mwuaji huamka asubuhi kukipambauka, huwaua maskini na wahitaji;Tena wakati wa usiku yu kama mwivi.
15. Tena jicho lake mzinifu hungojea wakati wa giza-giza,Akisema, Hapana jicho litakaloniona;Naye huuficha uso wake.
16. Wao hutoboa nyumba gizani;Hujifungia ndani wakati wa mchana;Hawaujui mwanga.
17. Kwani asubuhi kwao wote ni kama giza tupu;Kwani wao wavijua vitisho vya hiyo giza tupu.
18. Mwasema, Yeye ni mwepesi juu ya uso wa gharika;Sehemu yao inalaaniwa duniani;Hageuki kwenda njia ya mizabibuni.