Ayu. 23:8-14 Swahili Union Version (SUV)

8. Tazama, naenda mbele, wala hayuko;Narudi nyuma, lakini siwezi kumwona;

9. Na mkono wa kushoto, afanyapo kazi, lakini siwezi kumwona;Hujificha upande wa kuume, hata nisimwone.

10. Lakini yeye aijua njia niendeayo;Akisha kunijaribu, nitatoka kama dhahabu.

11. Mguu wangu umeshikamana sana na hatua zake;Njia yake nimeishika, wala sikukengeuka.

12. Sikurudi nyuma kuiacha amri ya midomo yake;Nimeyatunza maneno ya kinywa chake zaidi ya riziki yangu,

13. Lakini yeye ni mmoja, ni nani awezaye kumgeuza?Tena nafsi yake ilitakalo, ndilo afanyalo.

14. Kwani yeye hulitimiliza hilo nililoamuriwa;Tena mambo mengi kama hayo ya pamoja naye.

Ayu. 23