7. Hapo walekevu wangepata kuhojiana naye;Basi hivyo ningeachiliwa na mwamuzi wangu milele.
8. Tazama, naenda mbele, wala hayuko;Narudi nyuma, lakini siwezi kumwona;
9. Na mkono wa kushoto, afanyapo kazi, lakini siwezi kumwona;Hujificha upande wa kuume, hata nisimwone.
10. Lakini yeye aijua njia niendeayo;Akisha kunijaribu, nitatoka kama dhahabu.
11. Mguu wangu umeshikamana sana na hatua zake;Njia yake nimeishika, wala sikukengeuka.
12. Sikurudi nyuma kuiacha amri ya midomo yake;Nimeyatunza maneno ya kinywa chake zaidi ya riziki yangu,
13. Lakini yeye ni mmoja, ni nani awezaye kumgeuza?Tena nafsi yake ilitakalo, ndilo afanyalo.
14. Kwani yeye hulitimiliza hilo nililoamuriwa;Tena mambo mengi kama hayo ya pamoja naye.
15. Kwa hiyo naona taabu mbele ya uso wake;Nitakapofikiri, namwogopa.
16. Kwani Mungu ameufanya moyo wangu kuzimia,Naye Mwenyezi amenitaabisha;
17. Maana sikufadhaishwa kwa sababu ya giza,Wala kwa sababu giza kuu limenifunika uso.