1. Ndipo Ayubu akajibu, na kusema,
2. Hata leo mashitaka yangu yana uchungu;Pigo langu ni zito zaidi ya kuugua kwangu.
3. Laiti ningejua mahali niwezapo kumwona,Nifike hata hapo anapokaa!
4. Ningeiweka daawa yangu mbele yake,Na kukijaza kinywa changu hoja.
5. Ningeyajua maneno atakayonijibu,Na kuelewa na hayo atakayoniambia.
6. Je! Angeshindana nami kwa ukuu wa uwezo wake?La, lakini angenisikiliza.
7. Hapo walekevu wangepata kuhojiana naye;Basi hivyo ningeachiliwa na mwamuzi wangu milele.
8. Tazama, naenda mbele, wala hayuko;Narudi nyuma, lakini siwezi kumwona;