3. Je! Mwenyezi hupata furaha katika wewe kuwa mwenye haki?Au je, ni faida kwake, kwamba wafanya njia zako kuwa timilifu?
4. Je! Ni kwa wewe kumcha yeye anakukemea?Na kuingia hukumuni nawe?
5. Je! Uovu wako si mkuu?Wala maovu yako hayana mwisho.
6. Kwa kuwa umetwaa dhamana kwa nduguyo bure,Na kuwavua nguo zao walio uchi.
7. Hukumpa maji ya kunywa huyo aliyechoka,Nawe umemnyima chakula huyo mwenye njaa.
8. Lakini huyo shujaa, nchi ilikuwa yake;Na huyo mwenye kusifiwa, yeye aliikaa.
9. Umewafukuza wanawake wajane hali ya utupu,Na mikono ya mayatima imevunjwa.
10. Kwa hiyo umezungukwa na mitego,Na hofu ya ghafula yakutaabisha,
11. Au je! Huoni giza,Na maji mengi yanayokufunika?
12. Je! Mungu hayuko mbinguni juu?Tena tazama umbali wa nyota, jinsi zilivyo juu!
13. Nawe wasema, Mungu anajua nini?Je! Aweza kuamua kati ya giza kuu?
14. Mawingu mazito ni kifuniko chake, hata asione;Naye yuatembea juu ya kuba ya mbingu.
15. Je! Utaiandama njia ya zamaniWaliyoikanyaga watu waovu?
16. Ambao walinyakuliwa kabla ya wakati wao,Msingi wao ulimwagika kama kijito cha maji;
17. Waliomwambia Mungu, Tuondokee;Tena, Huyo Mwenyezi aweza kutufanyia nini?
18. Naye ndiye aliyezijaza nyumba zao vitu vyema;Lakini mashauri ya waovu na yawe mbali nami.
19. Wenye haki huyaona hayo wakafurahi;Nao wasio na hatia huwacheka;