Ayu. 22:16-22 Swahili Union Version (SUV)

16. Ambao walinyakuliwa kabla ya wakati wao,Msingi wao ulimwagika kama kijito cha maji;

17. Waliomwambia Mungu, Tuondokee;Tena, Huyo Mwenyezi aweza kutufanyia nini?

18. Naye ndiye aliyezijaza nyumba zao vitu vyema;Lakini mashauri ya waovu na yawe mbali nami.

19. Wenye haki huyaona hayo wakafurahi;Nao wasio na hatia huwacheka;

20. Wasema, Hakika hao waliotuinukia wamekatiliwa mbali,Na mabaki yao moto umeyateketeza.

21. Mjue sana Mungu, ili uwe na amani;Ndivyo mema yatakavyokujia.

22. Uyapokee, tafadhali, mafunzo yatokayo kinywani mwake,Na maneno yake yaweke moyoni mwako.

Ayu. 22