Ayu. 21:6-19 Swahili Union Version (SUV)

6. Hata nikumbukapo nahuzunika,Na utisho wanishika mwilini mwangu.

7. Mbona waovu wanaishi,Na kuwa wazee, naam, na kuongezeka kuwa na nguvu?

8. Kizazi chao kinathibitika nao machoni pao,Na wazao wao mbele ya macho yao.

9. Nyumba zao zi salama pasina hofu,Wala fimbo ya Mungu haiwapigi.

10. Fahali wao huvyaza wala hapungukiwi na nguvu;Ng’ombe wao mke huzaa, asiharibu mimba.

11. Huwatoa kama kundi watoto wao.Na watoto wao hucheza.

12. Huimba kwa matari na kwa kinubi,Na kuifurahia sauti ya filimbi.

13. Siku zao hutumia katika kufanikiwa,Kisha hushuka kuzimuni ghafula.

14. Walakini walimwambia Mungu. Tuondokee;Kwani hatutaki kuzijua njia zako.

15. Huyo Mwenyezi ni nani, hata tumtumikie?Nasi tutafaidiwa nini tukimwomba?

16. Tazama, kufanikiwa kwao hakumo mkononi mwao;Mashauri ya waovu na yawe mbali nami.

17. Je! Ni mara ngapi taa yao waovu huzimishwa?Na msiba wao kuwajilia?Na Mungu kuwagawanyia uchungu kwa hasira yake?

18. Ili wawe kama mabua makavu mbele ya upepo,Kama makapi yaliyochukuliwa na dhoruba?

19. Mwasema, Mungu huwawekea watoto wa mtu huo uovu wake.Na amlipe mwenyewe, ili apate kuujua.

Ayu. 21