3. Niacheni, nami pia nitanena;Tena nikiisha nena, zidini kudhihaki.
4. Mimi, je! Mashitaka yangu yamhusu mwanadamu?Nami kwa nini nisikose kusubiri?
5. Niangalieni, mkastaajabu,Mkaweke mkono kinywani.
6. Hata nikumbukapo nahuzunika,Na utisho wanishika mwilini mwangu.
7. Mbona waovu wanaishi,Na kuwa wazee, naam, na kuongezeka kuwa na nguvu?
8. Kizazi chao kinathibitika nao machoni pao,Na wazao wao mbele ya macho yao.
9. Nyumba zao zi salama pasina hofu,Wala fimbo ya Mungu haiwapigi.
10. Fahali wao huvyaza wala hapungukiwi na nguvu;Ng’ombe wao mke huzaa, asiharibu mimba.