26. Wao hulala mavumbini sawasawa,Mabuu huwafunika.
27. Tazama, nayajua mawazo yenu,Na mashauri mnayoazimia kwa uovu juu yangu.
28. Kwa kuwa mwasema, Nyumba ya huyo mkuu i wapi?Na hema waliyoikaa hao waovu i wapi?
29. Je! Hamkuwauliza wapitao njiani?Na maonyo yao hamyajui?
30. Kwamba mwovu huachiliwa katika siku ya msiba?Na kuongozwa nje katika siku ya ghadhabu?