1. Ndipo Ayubu akajibu, na kusema,
2. Yasikizeni sana maneno yangu;Jambo hili na liwe faraja yenu.
3. Niacheni, nami pia nitanena;Tena nikiisha nena, zidini kudhihaki.
4. Mimi, je! Mashitaka yangu yamhusu mwanadamu?Nami kwa nini nisikose kusubiri?
5. Niangalieni, mkastaajabu,Mkaweke mkono kinywani.
6. Hata nikumbukapo nahuzunika,Na utisho wanishika mwilini mwangu.