1. Ndipo Sofari, Mnaamathi, akajibu, na kusema,
2. Kwa hiyo mawazo yangu hunipa jawabu,Kwa ajili ya haraka niliyo nayo ndani yangu.
3. Nimesikia maonyo yanayonitahayarisha,Nayo roho ya ufahamu wangu hunijibu.
4. Je! Hujui neno hili tangu zamani za kale,Tangu wanadamu kuwekwa juu ya nchi,
5. Ya kuwa shangwe ya waovu ni kwa muda kidogo,Na furaha ya wapotovu ni ya dakika moja tu?
6. Ujapopanda ukuu wake mpaka mbinguni,Na kichwa chake kufikilia mawinguni;
7. Hata hivyo ataangamia milele kama mavi yake mwenyewe;Hao waliomwona watasema, Yuko wapi?
8. Ataruka mfano wa ndoto, asionekane;Naam, atafukuzwa kama maono ya usiku,