Ayu. 19:14-24 Swahili Union Version (SUV)

14. Watu wa mbari yangu wamekoma,Na rafiki zangu niwapendao wamenisahau.

15. Wakaao nyumbani mwangu, na vijakazi vyangu, wanihesabu kuwa mgeni;Mimi ni mgeni machoni pao.

16. Namwita mtumishi wangu, wala haniitikii,Ingawa namsihi kwa kinywa changu.

17. Pumzi zangu ni kama za mgeni kwa mke wangu,Nami ni machukizo kwa ndugu zangu.

18. Hata watoto wadogo hunidharau;Nikiondoka, huninena.

19. Wasiri wangu wote wanichukia;Na hao niliowapenda wamenigeukia.

20. Mfupa wangu unagandamana na ngozi yangu na nyama yangu,Nami nimeokoka na ngozi ya meno yangu tu.

21. Nihurumieni, nihurumieni, enyi rafiki zangu,Kwa maana mkono wa Mungu umenigusa.

22. Mbona ninyi mnaniudhi kama Mungu,Wala hamkutosheka na nyama yangu?

23. Laiti maneno yangu yangeandikwa sasa!Laiti yangeandikwa kitabuni!

24. Yakachorwa katika mwamba milele,Kwa kalamu ya chuma na risasi.

Ayu. 19