11. Tena ameziwasha ghadhabu zake juu yangu,Akanihesabia kuwa mmoja katika watesi wake.
12. Majeshi yake husongea pamoja, na kunipandishia njia yao,Na kupiga marago kuizunguka hema yangu.
13. Amewaweka ndugu zangu mbali nami,Na wanijuao wametengwa nami kabisa.
14. Watu wa mbari yangu wamekoma,Na rafiki zangu niwapendao wamenisahau.
15. Wakaao nyumbani mwangu, na vijakazi vyangu, wanihesabu kuwa mgeni;Mimi ni mgeni machoni pao.
16. Namwita mtumishi wangu, wala haniitikii,Ingawa namsihi kwa kinywa changu.
17. Pumzi zangu ni kama za mgeni kwa mke wangu,Nami ni machukizo kwa ndugu zangu.