8. Kwani ametupwa katika wavu na miguu yake mwenyewe,Naye huenda juu ya matanzi.
9. Tanzi litamshika kisigino chake,Na mtambo utamgwia.
10. Amefichiwa tanzi chini,Na mtego amewekewa njiani.
11. Matisho yatamtia hofu pande zote,Na kumfukuza karibu na visigino vyake.
12. Nguvu zake zitaliwa na njaa,Na msiba utakuwa tayari kwa kusita kwake.
13. Utakula via vya mwili wake,Naam, mzaliwa wa kwanza wa mauti atavila via vyake.
14. Atang’olewa katika hema yake aliyokuwa akiitumaini;Naye atapelekwa kwake mfalme wa utisho.
15. Ambacho si chake kitakaa katika hema yake;Kiberiti kitamwagwa juu ya makazi yake.