17. Kumbukumbu lake litakoma katika nchi,Wala hatakuwa na jina mashambani.
18. Atakimbizwa kutoka mwangani hata gizani,Na kufukuzwa atoke duniani.
19. Hatakuwa na mwana wala mjukuu kati ya watu wake,Wala hatasalia mtu hapo alipokaa.
20. Hao wanaokaa magharibi watastaajabia siku yake,Kama vile wanaokaa mashariki walivyotiwa hofu.
21. Hakika ndivyo yalivyo makazi ya wapotovu,Na hapa ni mahali pake asiyemjua Mungu.