12. Nguvu zake zitaliwa na njaa,Na msiba utakuwa tayari kwa kusita kwake.
13. Utakula via vya mwili wake,Naam, mzaliwa wa kwanza wa mauti atavila via vyake.
14. Atang’olewa katika hema yake aliyokuwa akiitumaini;Naye atapelekwa kwake mfalme wa utisho.
15. Ambacho si chake kitakaa katika hema yake;Kiberiti kitamwagwa juu ya makazi yake.
16. Chini, mizizi yake itakaushwa;Na juu, tawi lake litasinyaa.
17. Kumbukumbu lake litakoma katika nchi,Wala hatakuwa na jina mashambani.