1. Ndipo Bildadi, Mshuhi, akajibu, na kusema,
2. Je! Hata lini utayategea maneno mitambo?Fikiri, kisha baadaye tutanena.
3. Twahesabiwa kuwa wanyama kwa sababu gani,Tena kuwa wanajisi machoni pako?
4. Wewe ujiraruaye mwenyewe katika hasira yako,Je! Dunia itaachwa kwa ajili yako wewe?Au jabali litaondolewa mahali pake?
5. Naam, mwanga wa waovu utazimika,Wala mwali wa moto wake hautang’aa.
6. Mwanga hemani mwake utakuwa giza,Nayo taa iliyo juu yake itazimishwa.
7. Hatua zake za nguvu zitasongwa,Na shauri lake mwenyewe litamwangusha chini.
8. Kwani ametupwa katika wavu na miguu yake mwenyewe,Naye huenda juu ya matanzi.
9. Tanzi litamshika kisigino chake,Na mtambo utamgwia.