8. Walekevu watayastaajabia hayo,Na asiye na hatia atajiamsha juu ya mpotovu.
9. Lakini mwenye haki ataishika njia yake,Naye mwenye mikono safi atazidi kupata nguvu.
10. Lakini rudini; ninyi nyote, njoni sasa;Wala sitampata mtu mwenye hekima kati yenu.
11. Siku zangu zimepita, makusudi yangu yamevunjika,Hata hayo niliyo nayo moyoni mwangu.
12. Wabadili usiku kuwa mchana;Wasema, Mwanga u karibu kwa sababu ya giza.
13. Nikitazamia kuzimu kuwa nyumba yangu;Nikitandika malazi yangu gizani;
14. Ikiwa nimeuita uharibifu, Wewe u baba yangu;Na kuliambia buu, Wewe u mama yangu, na umbu langu;
15. Basi, tumaini langu li wapi?Na tumaini langu, ni nani atakayeliona?
16. Litashuka kwenye makomeo ya kuzimu,Itakapokuwapo raha mavumbini.