1. Roho yangu imezimika, siku zangu zimekoma,Kaburi i tayari kunipokea.
2. Ni kweli wako kwangu wenye kufanya dhihaka,Jicho langu hukaa katika kunifanyia uchungu kwao.
3. Nipe rehani basi, uwe dhamana kwa ajili yangu kwako wewe mwenyewe;Kuna nani atakayeniwekea dhamana?
4. Kwani mioyo yao imeificha ufahamu;Kwa hiyo hutawakuza.
5. Awafitiniye rafiki zake wawe mawindo,Hata macho ya watoto wake yataingia kiwi.
6. Amenifanya niwe simo kwa watu;Nimekuwa mwenye kuchukiwa kwa wazi.
7. Jicho langu nalo limekuwa giza kwa sababu ya majonzi,Na via vyangu vyote vimekuwa kama kivuli.
8. Walekevu watayastaajabia hayo,Na asiye na hatia atajiamsha juu ya mpotovu.