1. Roho yangu imezimika, siku zangu zimekoma,Kaburi i tayari kunipokea.
2. Ni kweli wako kwangu wenye kufanya dhihaka,Jicho langu hukaa katika kunifanyia uchungu kwao.
3. Nipe rehani basi, uwe dhamana kwa ajili yangu kwako wewe mwenyewe;Kuna nani atakayeniwekea dhamana?
4. Kwani mioyo yao imeificha ufahamu;Kwa hiyo hutawakuza.
5. Awafitiniye rafiki zake wawe mawindo,Hata macho ya watoto wake yataingia kiwi.
6. Amenifanya niwe simo kwa watu;Nimekuwa mwenye kuchukiwa kwa wazi.