19. Hata sasa, tazama, shahidi wangu yuko mbinguni.Na huyo atakayenidhamini yuko juu.
20. Rafiki zangu hunidharau;Lakini jicho langu humwagia Mungu machozi;
21. Laiti angemtolea mtu hoja mbele ya Mungu,Amtetee na mwanadamu mbele ya jirani yake.
22. Kwani ikiisha pita miaka michache,Nitakwenda njia hiyo ambayo sitarudi tena.