10. Wamenifumbulia vinywa vyao;Wamenipiga shavuni kwa kunitukana;Hujikutanisha pamoja juu yangu.
11. Mungu amenitia kwa hao wapotovu,Na kunitupa mikononi mwao waovu.
12. Nilikuwa katika raha, naye akanivunja-vunja;Naam, amenishika shingo, na kuniponda;Tena amenisimamisha niwe shabaha yake.
13. Wapigaji wake wa mishale hunizingira kotekote,Hunipasua viuno vyangu, asinihurumie;Nyonga zangu amezimwaga juu ya nchi.
14. Hunivunja kwa uvunjifu juu ya uvunjifu;Hunishambulia mfano wa jitu shujaa.
15. Nimeshona nguo ya magunia juu ya mwili wangu,Na pembe yangu nimeidhili uvumbini.
16. Uso wangu umeharibika kwa kutoa machozi,Na giza tupu li katika kope zangu;
17. Ijapokuwa hapana jeuri mikononi mwangu,Na kuomba kwangu ni safi.
18. Ee nchi, usiifunike damu yangu,Na kilio changu kisipate mahali pa kupumzika.