14. Je! Mwanadamu ni kitu gani, hata akawa safi?Huyo aliyezaliwa na mwanamke, hata awe na haki?
15. Yeye hawategemei watakatifu wake;Naam, mbingu nazo si safi machoni pake.
16. Sembuse mtu ambaye ni mwenye kuchukiza na uchafu,Mwanadamu anywaye uovu kama anywavyo maji!
17. Mimi nitakuonyesha, unisikilize;Na hayo yote niliyoyaona nitayanena;
18. (Ambayo watu wenye hekima wameyatangazaTokea baba zao, wala hawakuyaficha;
19. Waliopewa hiyo nchi peke yao,Wala mgeni hakupita kati yao);
20. Mtu mwovu huwa na uchungu siku zake zote,Hata hesabu ya miaka aliyowekewa mwenye kuonea.
21. Sauti za utisho zi masikioni mwake;Katika kufanikiwa kwake mtekaji nyara atamjia juu yake;
22. Yeye hasadiki kwamba atarudi kutoka gizani,Naye hungojewa na upanga;