Ayu. 15:10-23 Swahili Union Version (SUV)

10. Wenye mvi, na walio wazee sana, wote wapo pamoja nasi,Ambao ni wazee kuliko baba yako.

11. Je! Utulizi wa Mungu ni mdogo sana kwako,Na hilo neno la upole si kitu kwako?

12. Mbona moyo wako unakutaharakisha!Na macho yako, je! Kwani kung’ariza?

13. Hata ukageuza roho yako iwe kinyume cha Mungu,Na kuyatoa maneno kama hayo kinywani mwako.

14. Je! Mwanadamu ni kitu gani, hata akawa safi?Huyo aliyezaliwa na mwanamke, hata awe na haki?

15. Yeye hawategemei watakatifu wake;Naam, mbingu nazo si safi machoni pake.

16. Sembuse mtu ambaye ni mwenye kuchukiza na uchafu,Mwanadamu anywaye uovu kama anywavyo maji!

17. Mimi nitakuonyesha, unisikilize;Na hayo yote niliyoyaona nitayanena;

18. (Ambayo watu wenye hekima wameyatangazaTokea baba zao, wala hawakuyaficha;

19. Waliopewa hiyo nchi peke yao,Wala mgeni hakupita kati yao);

20. Mtu mwovu huwa na uchungu siku zake zote,Hata hesabu ya miaka aliyowekewa mwenye kuonea.

21. Sauti za utisho zi masikioni mwake;Katika kufanikiwa kwake mtekaji nyara atamjia juu yake;

22. Yeye hasadiki kwamba atarudi kutoka gizani,Naye hungojewa na upanga;

23. Hutanga-tanga ili apate chakula, akisema, Ki wapi?Ajua kwamba siku ya giza i tayari karibu yake;

Ayu. 15