1. Ndipo Elifazi, Mtemani, akajibu, na kusema,
2. Je! Yapasa mtu mwenye hekima kujibu kwa ujuzi wa uvuvio,Na kujaza tumbo lake na upepo wa mashariki?
3. Je! Ahoji na mazungumzo yasiyo faida,Au kwa maneno ambayo hawezi kufanya mema kwayo?
4. Naam, wewe waondoa kicho,Nawe wazuia ibada mbele za Mungu.
5. Kwani uovu wako unakufundisha kinywa chako,Nawe wachagua ulimi wake mwenye hila.
6. Kinywa chako mwenyewe chakuhukumia makosa, wala si mimi;Naam, midomo yako mwenyewe hushuhudia juu yako.
7. Je! Wewe u mtu wa kwanza aliyezaliwa?Au, ulizawa wewe kabla ya milima?
8. Je! Umesikia mashauri ya siri ya Mungu?Nawe je! Wazuia hekima iwe yako tu?
9. Je! Wewe wajua neno lipi, ambalo sisi hatulijui?Nawe wafahamu nini, ambalo halimo ndani yetu?
10. Wenye mvi, na walio wazee sana, wote wapo pamoja nasi,Ambao ni wazee kuliko baba yako.
11. Je! Utulizi wa Mungu ni mdogo sana kwako,Na hilo neno la upole si kitu kwako?