5. Kwa kuwa siku zake zimeamriwa, hesabu ya miezi yake unayo wewe,Nawe umemwekea mipaka yake asiyoweza kuipita;
6. Acha kumwangalia yeye, apate kupumzika,Hata atakapoitimiza siku yake, kama aliyeajiriwa.
7. Kwani yako matumaini ya mti, ya kuwa ukikatwa utachipuka tena,Wala machipukizi yake hayatakoma.
8. Ijapokuwa mizizi yake huchakaa mchangani,Na shina lake kufa katika udongo;
9. Lakini kwa harufu ya maji utachipuka,Na kutoa matawi kama mche.
10. Lakini mwanadamu hufa, huifariki dunia;Naam, mwanadamu hutoa roho, naye yupo wapi?
11. Kama vile maji kupwa katika bahari,Na mto kupunguka na kukatika;
12. Ni vivyo mwanadamu hulala chini, asiinuke;Hata wakati wa mbingu kutokuwako tena, hawataamka,Wala kuamshwa usingizini.