1. Mwanadamu aliyezaliwa na mwanamkeSiku zake za kuishi si nyingi, naye hujaa taabu.
2. Yeye huchanua kama vile ua, kisha hukatwa;Hukimbia kama kivuli, wala hakai kamwe.
3. Nawe, je! Wafumbua macho yako kumwangalia mtu kama yeye,Na kunitia katika hukumu pamoja nawe?
4. Ni nani awezaye kutoa kitu kilicho safi kitoke katika kitu kichafu? Hapana awezaye.
5. Kwa kuwa siku zake zimeamriwa, hesabu ya miezi yake unayo wewe,Nawe umemwekea mipaka yake asiyoweza kuipita;
6. Acha kumwangalia yeye, apate kupumzika,Hata atakapoitimiza siku yake, kama aliyeajiriwa.
7. Kwani yako matumaini ya mti, ya kuwa ukikatwa utachipuka tena,Wala machipukizi yake hayatakoma.