Ayu. 13:25-28 Swahili Union Version (SUV)

25. Je! Utalitaabisha jani lipeperushwalo?Au, je! Utayafuatia hayo mabua makavu?

26. Kwani umeandika maneno ya uchungu juu yangu,Na kunirithisha maovu ya ujana wangu;

27. Waitia miguu yangu katika mkatale, na kuyaaua mapito yangu yote;Wajiandikia alama kuzizunguka nyayo za miguu yangu;

28. Nijapokuwa ni kama kitu kilichooza, kinachosinyaa,Mfano wa nguo iliyoliwa na nondo.

Ayu. 13