Ayu. 13:17-27 Swahili Union Version (SUV)

17. Sikieni sana maneno yangu,Maelezo yangu na yaingie masikioni mwenu.

18. Angalieni sasa, nimekwisha kulitengeneza neno langu,Najua ya kuwa ni mwenye haki mimi.

19. Yuko nani atakayeshindana nami?Maana sasa nitanyamaa kimya na kutoa roho.

20. Lakini msinifanyie mambo mawili, hayo tu,Ndipo nami sitajificha usoni pako;

21. Uondoe mkono wako usinilemee;Na utisho wako usinitie hofu.

22. Basi uite wakati huo, nami nitaitika;Au, niache ninene mimi, nawe unijibu.

23. Maovu yangu na dhambi zangu ni ngapi?Nijulishe kosa langu na dhambi yangu.

24. Mbona umeuficha uso wako,Na kunihesabu kuwa ni adui yako?

25. Je! Utalitaabisha jani lipeperushwalo?Au, je! Utayafuatia hayo mabua makavu?

26. Kwani umeandika maneno ya uchungu juu yangu,Na kunirithisha maovu ya ujana wangu;

27. Waitia miguu yangu katika mkatale, na kuyaaua mapito yangu yote;Wajiandikia alama kuzizunguka nyayo za miguu yangu;

Ayu. 13