Ayu. 13:1-4 Swahili Union Version (SUV)

1. Tazama, jicho langu limeyaona hayo yote,Sikio langu limeyasikia na kuelewa nayo.

2. Hayo myajuayo ninyi, na mimi pia nayajua;Mimi si duni kuliko ninyi.

3. Hakika ningenena naye huyo Mwenyezi,Nami nataka kuhojiana na Mungu.

4. Lakini ninyi hubuni maneno ya uongo,Ninyi nyote ni matabibu wasiofaa.

Ayu. 13