Ayu. 11:1-9 Swahili Union Version (SUV)

1. Ndipo Sofari Mnaamathi akajibu, na kusema,

2. Je! Huu wingi wa maneno usijibiwe?Na mtu aliyejaa maneno, je! Ahesabiwe kuwa na haki?

3. Je! Majivuno yako yawanyamazishe watu wawe kimya?Nawe hapo ufanyapo dhihaka, je! Hapana mtu atakayekutahayarisha?

4. Kwa kuwa wewe wasema, Mafunzo yangu ni safi,Nami ni safi machoni pako.

5. Lakini, laiti Mungu angenena,Na kuifunua midomo yake juu yako;

6. Tena akuonyeshe hizo siri za hekima,Ya kuwa hufanikiwa katika kuyatimiza makusudi yake!Ujue basi ya kuwa Mungu akuachilia katika uovu wako.

7. Je! Wewe waweza kuuvumbua ukuu wa Mungu?Waweza kuufikilia upeo wa huyo Mwenyezi?

8. Ni juu mno kama mbingu; waweza kufanya nini wewe?Ni wenye kina kuliko kuzimuni; waweza kujua nini wewe?

9. Cheo chake ni kirefu kuliko dunia,Ni kipana zaidi ya bahari.

Ayu. 11