Ayu. 10:15-22 Swahili Union Version (SUV)

15. Mimi nikiwa mbaya, ole wangu!Nami nikiwa mwenye haki, walakini sitainua kichwa changu;Mimi nimejaa aibuNa kuyaangalia mateso yangu.

16. Kichwa changu kikijiinua, waniwinda kama simba;Tena wajionyesha kwangu kuwa wa ajabu.

17. Wewe warejeza upya hao mashahidi yako juu yangu,Na kasirani yako waiongeza juu yangu;Jeshi kwa jeshi juu yangu.

18. Kwa nini basi kunitoa tumboni?Ningekata roho, lisinione jicho lo lote.

19. Ningalikuwa kama mtu asiyekuwapo;Ningalichukuliwa kaburini kutoka tumboni.

20. Je! Siku zangu si chache? Acha basi,Usinisumbue, nipate ngaa kutuzwa moyo kidogo.

21. Kabla sijaenda huko ambako sitarudi kutoka huko tena,Ni hiyo nchi ya giza, giza tupu;

22. Ni nchi ya giza kuu, kama giza lenyewe lilivyo;Ni nchi ya giza tupu, isiyo na matengezo ya mambo yo yote,Nchi ambayo nuru yake ni kama giza.

Ayu. 10