Ayu. 10:12-18 Swahili Union Version (SUV)

12. Umenijazi uhai na upendeleo,Na maangalizi yako yameilinda roho yangu.

13. Lakini mambo haya uliyaficha moyoni mwako;Najua kuwa haya yamo nafsini mwako;

14. Nikifanya dhambi, ndipo waniangalia,Wala hutaniachilia na uovu wangu.

15. Mimi nikiwa mbaya, ole wangu!Nami nikiwa mwenye haki, walakini sitainua kichwa changu;Mimi nimejaa aibuNa kuyaangalia mateso yangu.

16. Kichwa changu kikijiinua, waniwinda kama simba;Tena wajionyesha kwangu kuwa wa ajabu.

17. Wewe warejeza upya hao mashahidi yako juu yangu,Na kasirani yako waiongeza juu yangu;Jeshi kwa jeshi juu yangu.

18. Kwa nini basi kunitoa tumboni?Ningekata roho, lisinione jicho lo lote.

Ayu. 10