1. Nafsi yangu inachoka na maisha yangu;Sitajizuia na kuugua kwangu;Nitanena kwa uchungu wa roho yangu.
2. Nitamwambia Mungu, Usinihukumie makosa;Nionyeshe sababu ya wewe kushindana nami.
3. Je! Ni vema kwako wewe kuonea,Na kuidharau kazi ya mikono yako,Na kuyaangazia mashauri ya waovu?
4. Je! Wewe una macho ya kimwili,Au je! Waona kama aonavyo binadamu?
5. Je! Siku zako ni kama siku za mtu,Au je! Miaka yako ni kama siku za mtu,
6. Hata ukauliza-uliza habari za uovu wangu,Na kuitafuta dhambi yangu,
7. Ujapojua ya kuwa mimi si mwovu;Wala hapana awezaye kuokoa na mkono wako?
8. Mikono yako imeniumba na kunifinyanga;Nawe utageuka na kuniangamiza?
9. Kumbuka, nakusihi ulivyonifinyanga kama vile udongo;Nawe, je! Utanirudisha uvumbini tena?
10. Je! Wewe hukunimimina kama maziwa,Na kunigandisha mfano wa jibini?