Amu. 9:9-11 Swahili Union Version (SUV)

9. Lakini huo mzeituni ukaiambia, Je! Niache mafuta yangu, ambayo kwangu mimi watu wamheshimu Mungu na wanadamu, ili niende nikayonge-yonge juu ya miti?

10. Kisha miti ikauambia mtini, Njoo wewe, utawale juu yetu.

11. Lakini huo mtini ukaiambia, Je! Niuache utamu wangu, na matunda yangu mazuri, niende nikayonge-yonge juu ya miti?

Amu. 9