2 Tim. 4:1-7 Swahili Union Version (SUV)

1. Nakuagiza mbele za Mungu, na mbele za Kristo Yesu, atakayewahukumu walio hai na waliokufa; kwa kufunuliwa kwake na kwa ufalme wake;

2. lihubiri neno, uwe tayari, wakati ukufaao na wakati usiokufaa, karipia, kemea, na kuonya kwa uvumilivu wote na mafundisho.

3. Maana utakuja wakati watakapoyakataa mafundisho yenye uzima; ila kwa kuzifuata nia zao wenyewe watajipatia waalimu makundi makundi, kwa kuwa wana masikio ya utafiti;

4. nao watajiepusha wasisikie yaliyo kweli, na kuzigeukia hadithi za uongo.

5. Bali wewe, uwe na kiasi katika mambo yote, vumilia mabaya, fanya kazi ya mhubiri wa Injili, timiliza huduma yako.

6. Kwa maana, mimi sasa namiminwa, na wakati wa kufariki kwangu umefika.

7. Nimevipiga vita vilivyo vizuri, mwendo nimeumaliza, Imani nimeilinda;

2 Tim. 4