2 Tim. 2:4-15 Swahili Union Version (SUV)

4. Hakuna apigaye vita ajitiaye katika shughuli za dunia, ili ampendeze yeye aliyemwandika awe askari.

5. Hata mtu akishindana katika machezo hapewi taji, asiposhindana kwa halali.

6. Yampasa mkulima mwenye taabu ya kazi kuwa wa kwanza wa kupata fungu la matunda.

7. Yafahamu sana hayo nisemayo, kwa maana Bwana atakupa akili katika mambo yote.

8. Mkumbuke Yesu Kristo, aliyefufuka katika wafu, wa uzao wa Daudi kama inenavyo injili yangu.

9. Nami katika hiyo nimeteswa hata kufungwa kama mtenda mabaya; lakini neno la Mungu halifungwi.

10. Kwa ajili ya hilo nastahimili mambo yote, kwa ajili ya wateule, ili wao nao waupate wokovu ule ulio katika Kristo Yesu, pamoja na utukufu wa milele.

11. Ni neno la kuaminiwa. Kwa maana,Kama tukifa pamoja naye,tutaishi pamoja naye pia;

12. Kama tukistahimili,tutamiliki pamoja naye;Kama tukimkana yeye,yeye naye atatukana sisi;

13. Kama sisi hatuamini,yeye hudumu wa kuaminiwa.Kwa maana hawezi kujikana mwenyewe.

14. Uwakumbushe mambo hayo, ukiwaonya machoni pa Mungu, wasiwe na mashindano ya maneno, ambayo hayana faida, bali huwaharibu wasikiao.

15. Jitahidi kujionyesha kuwa umekubaliwa na Mungu, mtenda kazi asiye na sababu ya kutahayari, ukitumia kwa halali neno la kweli.

2 Tim. 2